Friday, 9 January 2015

CUF inavyotumia Escrow kama silaha ya kuiangamiza CCM Kusini

Wapinzani wamekusudia kuikwamisha Katiba Inayopendekezwa huku wakielekeza nguvu zao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa lengo la kukiangusha chama tawala.
Mwaka huu una matukio makuu mawili ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi ili kuandika historia; upigaji kura wa kukubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.Mambo hayo yanasababisha wanasiasa na vyama vyao kuwa katika hekaheka kubwa ili kuhakikisha wanashinda katika matukio hayo kulingana na msimamo wao.
Kumekuwapo na mgawanyiko katika suala la kuikubali au kuikataa katiba hiyo na mvutano mkubwa upo kati ya Serikali kwa maana chama tawala cha CCM na wapinzani chini ya muungano wao wa vyama vitatu, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Silaha kubwa wanayoitumia Ukawa kwa sasa katika kuikabili CCM ni kashfa ya ufisadi ya Akaunti Tegeta Escrow na msimamo kwamba hawaiungi mkono Katiba Inayopendekezwa.
Kutokana na hali hiyo, CUF imefanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara ambako ilitumia silaha hizo katika kushawishi wananchi kuiunga mkono.
Katika mkutano huo, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alimwalika mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ambaye kamati yake ndiyo ilishughulikia sakata hilo kwa kutumia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Ulikuwa ni mkutano uliopambwa na shangwe na nderemo za kila aina kutoka kwa wafuasi wa CUF waliojitokeza kuwalaki kwenye Daraja za Mikindani na kufanya maandamano ya zaidi ya magari 30, pikipiki 300 na bajaji 40 na pikipiki huku wananchi wakiwa wamejipanga kwenye mistari barabarani.
Baadhi walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali, zikiwemo zilizokuwa na kibwagizo cha “tunataka fedha zetu za Escrow zirudi... Mtumbwi wa Chenge umetoboka”. Andrew Change ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) alitumia mkutano huo kuwaomba wananchi wa mkoa huo kupiga kura ya ‘hapana’ kwa Katiba Inayopendekezwa wakati muda utakapofika.
Alisema Chenge na wabunge wenzake wa CCM wametengeneza Katiba inayoendelea kulinda maslahi ya wachache badala ya Watanzania wote.
“Ikiletwa hapa katiba ya Chenge ikataeni. Ikataeni, tupeni kule kwani mkiikubali mtakuwa mnaungana na mafisadi kuhalalisha vitendo vya kifisadi viendelee.

“Fanyeni hivyo kwa maana maoni yenu yametupwa. Nanyi itupeni Katiba yao kwa kupiga kura ya hapana kwa wingi.
“Lakini hilo litaanza na ninyi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura litakapoanza, bila hivyo hatutaweza kuipinga,” anasema Mnyaa.
Alisema: “CUF itakuwa nanyi bega kwa bega katika hili kwani tulitarajia kupata Katiba bora lakini imekuwa kinyume chake na hili halina ubishi kwani mlijionea ninyi wenyewe yaliyokuwa yanaendelea kuwa bungeni Dodoma.”
Profesa Lipumba aliwaomba wananchi waiunge mkono CUF kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu na akawashukuru kwa jinsi walivyokiunga mkono chama hicho kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika hivi karibuni.
“Wananchi wametuamini na kutuchagua sasa kazi ni kwetu kuwatumikia kwa weledi na kuonyesha tofauti yetu na walio kuwapo... Ongozeni kwa misingi ya chama kwa haki sawa kwa wote,” anasema.
Anaongeza: “Harakati za kuiondoa CCM madarakani imefika. Utakapofika wakati wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura hakikisheni mnajitokeza kwa wingi ili muwe na fursa ya kuchagua na kuitupilia mbali CCM.”
Profesa Lipumba anasema, “Mabadiliko ya nchi hii yatafanywa na sisi wenyewe kama tutaamua. Dalili tayari mmeanza kuzionyesha mabadiliko kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Endeleeni hivyo hivyo kwani CCM imeshindwa na sasa haina uwezo tena wa kuendelea kutuongoza.”
 Zitto na Escrow
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, ambaye ni mbunge kupitia Chadema, alieleza kwenye mkutano huo jinsi kamati yake ilivyofichua uozo katika sakata la escrow.
Anasema wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow ulikuwa ni Sh306 bilioni na kusisitiza ni lazima zirejeshwe ingawa Rais Jakaya Kikwete wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka jana alisema siyo mali ya umma bali ni za IPTL.
“Serikali lazima ichukue hatua mara moja kuhakikisha fedha zilizokuwamo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow Anarudi, uamuzi wa mahakama ya kimataifa unatekelezwa na fedha za umma zinarejeshwa Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) na zile za binafsi zinalipwa kwa wamiliki halali.

Jaji Manento: Sitasahau mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi

Dar es Salaam. Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento amesema jambo kubwa alilolipitia wakati wa uongozi wake lilikuwa ni kifo cha mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi baada ya kupigwa bomu na polisi, mkoani Iringa mwaka 2012.
Alisema jambo hilo lilikuwa kubwa kwa wananchi kuliko lilivyopokelewa na Serikali. Alisisitiza kuwa tume yake ilitoa taarifa ya kifo hicho ikiwa na mapendekezo na kuikabidhi Serikali. Jambo la kushangaza, alisema mapendekezo yao hayajatekelezwa mpaka leo.
“Hili jambo kwangu lilikuwa kubwa. Tume tulifuatilia tukio lile na kubaini kuwa Mwangosi alipigwa bomu na polisi. Tulitoa mapendekezo yetu, lakini mpaka leo hakuna utekelezaji wake,” alisema Manento ambaye pia ni Jaji Kiongozi mstaafu.
Aliongeza kuwa sasa ni kazi ya Nyanduga kufuatilia utekelezaji wa maazimio yale ili kuhakikisha haki inatendeka na kujenga imani ya tume kwa wananchi.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 129 (1)(c) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria ya Haki za Binadamu na Utawala Bora namba saba ya mwaka 2001.
Jukumu kubwa la tume hii ni kulinda, kutetea na kuhifadhi haki za binadamu nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo, tume imepewa mamlaka ya kupokea malalamiko kutoka sehemu mbalimbali na kuanzisha uchunguzi wake yenyewe kama itaona kuna ukiukwaji wa haki.
Tume ya Haki za Binadamu ilitoa mapendekezo matano wakati wa taarifa yake juu ya kifo cha Mwangosi. Baadhi ya mapendekezo hayo yalikuwa ni: elimu ya vyama vya siasa na sheria ya polisi kuhusu vyama vya siasa kutolewa kwa askari polisi, ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa.
Maoni mengine yalikuwa ni: Jeshi la polisi na msajili wa vyama vya siasa kuepuka kufanya maamuzi ambayo yatasababisha hisia za ubaguzi au upendeleo miongoni mwa jamii wakati wanatekeleza majukumu yao.
Kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya, zilitakiwa kuwa makini na vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali kwenye maeneo yao.
Pia, tume ilipendekeza kuheshimiwa na kulindwa kwa misingi ya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Awali, Rais Kikwete alimwapisha Msajili wa Mahakama ya Rufani, Katarina Revocati ambaye aliahidi kuendeleza nguvu iliyoanzishwa ya kuleta mabadiliko katika mhimili wa Mahakama na kuufanya utende kazi zake kwa ufanisi.
“Baada ya mabadiliko ya sheria, ofisi ya msajili imebaki na kazi ya kushughulikia mashauri tu. Kuanzia mwaka jana majaji walianza kuzunguka mikoani kusikiliza kesi za muda mrefu. Nina tumaini nitasaidia kuongeza nguvu katika mpango huo,” alisema.
Alitaja changamoto kubwa iliyo mbele yake kuwa ni mlundikano wa kesi nchi nzima bila kusikilizwa.
Alisema hatua zimeshachukuliwa kukabiliana na tatizo hilo na kuwa majaji walianza na mikoa ya Tabora na Dar es Salaam.
Naye mwenyekiti mpya wa tume hiyo, Bahame Nyanduga alisema tume itashirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na asasi za kiraia katika kusimamia haki za binadamu hasa mwaka huu wa uchaguzi mkuu.
Nyanduga aliyasema hayo jana baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam kushika wadhifa huo. Sambamba naye, pia aliapishwa Makamu Mwenyekiti, Iddi Mapuri na makamishna wanne ambao ni Mohamed Hamad, Kelvin Mandopi, Rehema Ntimizi na Salma Hassan.
“Katika uongozi wangu, nitashirikiana na wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bora ili kujenga jamii ya Watanzania katika msingi wa haki na usawa.

Kenge 140 wanaswa JNIA wakitoroshwa nje ya nchi

Dar es Salaam.  Jeshi la Polisi la   Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa uwanjani hapo jana  majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa  na safari ya  kuelekea nchini Kuwait  kupitia Dubai  na Shirika la Ndege la Emirates  .
Kamanda  Selemani alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi  kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.
“Kenge waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge 15 na mifuko mingine walikaa wawili,”alisema kamanda Selemani.

Pinda aionya CCM uteuzi wa wagombea


Katavi. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amezitaka ngazi mbalimbali za uteuzi wa wagombea wa CCM kuwapa wananchi nafasi kuchagua watu wanaowataka ili kuepuka kupoteza viti katika uchaguzi.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mikutano wa Kashaulili, Mpanda mkoani hapa.
Pia alitumia mkutano huo kuaga jimboni humo akisema muda wa kuendelea kuwa Mbunge wa Katavi umetosha na sasa anatafuta kitu kingine cha kufanya.
Kwa mara ya kwanza, Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge wa Mpanda Mashariki (sasa Katavi) mwaka 2000 na ameongoza jimbo hilo kwa mihula mitatu.
Kuhusu uteuzi
Akizungumzia uteuzi wa wagombea mbalimbali, Pinda aliwaasa viongozi wa CCM kuwateua watu wanaofaa kugombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali wale ambao wanakubalika na wananchi na wawape nafasi wananchi kuchagua mtu wanayemtaka.
Alisema haifai CCM kuwalazimisha kwa kuwachagulia wananchi kiongozi wasiyemtaka... “Kumekuwa na tabia ya kuteua watu ambao hawakubaliki kwa wananchi na matokeo yake watu hao wamekuwa wakishindwa kwenye uchaguzi... acheni chuki, msiteue watu kuwania uongozi kwa ajili ya kupewa pesa na urafiki,” alisema.
Pinda aliyetangaza ni ya kuwania urais kimyakimya, aliwataka Watanzania kutowachagua watu wanaotaka kiti hicho na vile vya ubunge na udiwani kwa kutanguliza fedha.
“Watu hao wanaotafuta uongozi kwa kutoa rushwa kwa wananchi ni hatari, kuweni makini kwa kuchagua viongozi waadilifu watakaoongoza kwa kutanguliza mbele utaifa kuliko masilahi yao binafsi.
“Wako watu wanaotaka uongozi kwa kuhonga wapigakura, watu wa namna hiyo hawafai kuwa wagombea wa urais, ubunge na udiwani kwa kuwa si waadilifu na wakishapata uongozi kamwe hawezi kuwajali wananchi kwanza watataka kurudisha fedha walizotoa.
“Hakikisheni mnachagua viongozi ambao wanaweza kuwaongoza kwenye maeneo yenu na siyo vinginevyo, achaneni na watu wanaowapa pesa hao hawatawapeleka kokote badala yake watakuwa viongozi wabinafsi kwa kutanguliza masilahi yao mbele na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani,” alisema Pinda.
Alisema: “Watu wanaotaka uongozi kwa fedha, wanapowaletea hizo pesa kuleni lakini mhakikishe wakati wa uchaguzi hamwapigii kura.”
Huku akishangiliwa na wananchi hao kwa makofi na vigelegele, alisisitiza: “Ukitaka kumchagua mtu mwenye sifa za kuwa rais wa nchi hii, chagueni mtu ambaye hatoi rushwa kwa wananchi, mwadilifu, mnyenyekevu na mchapakazi. Hata watu wanaotaka ubunge na udiwani hakikisheni hamwachagui wanaotaka uongozi kwa rushwa, chagueni viongozi watakaowaongoza vizuri kwenye maeneo yenu.”
Viongozi wa dini
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa dini kuachana na masuala ya kuhubiri siasa wanapokuwa kwenye nyumba za ibada na badala yake wafanye kazi wanayotakiwa kufanya ya kuhubiria neno la Mungu.
“Kumeanza kusikika maneno kuwa viongozi wa dini wanaendeleza chuki kwa kuhubiri siasa kwenye nyumba za ibada badala ya kutenda kazi zao za kuwapa neno la Mungu waumini wao.
“Viongozi hawa wajibu wao ni kufanya kazi ya kuwaongoza waumini kwa kuwahubiria neno la Mungu kuliko kutumia nyumba za ibada kuhubiri siasa, kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi zao.
“Kama wanataka kufanya siasa waje hapa majukwaani tupambane sawasawa... kama mtu anaweza aje apambane hapa,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema viongozi wa dini washirikiane na Serikali na chama hasa tawala (CCM), katika kuhubiri upendo na amani lakini si siasa.
“Ninaogopa kuona kiongozi wa dini anakwenda kanisani kisha anasema chagueni Chama cha Mapinduzi, ni hatari. Nafasi walizonazo ni za kidini na zinatakiwa kuheshimiwa,” alisema na kuongeza kuwa kuacha hayo yakiendelea ni hatari kwa Taifa kwani na kunaweza kuleta mgogoro katika jamii.
Waziri Mkuu leo anakamilisha ziara yake mkoani Katavi kwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ifukutwa, Mpanda.

Hukumu CCM ndani ya saa 72

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya CCM, itakuwa na vikao vizito kuanzia Jumatatu kujadili masuala mbalimbali yanayokikabili chama hicho.
Mambo makubwa yanayotarajiwa kuchukua nafasi katika vikao hivyo vitakavyoanza saa 72 zijazo ni kuwajadili wanachama wake ambao baadhi ni mawaziri waliokumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow na tathmini ya wanachama wake sita walio katika adhabu ya mwaka mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kudaiwa kufanya kampeni za urais kabla ya muda.
Pia kamati hiyo, inatarajia kutumia vikao hivyo kuangalia namna ya kupata wagombea watakaokubalika na wananchi kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Monday, 5 January 2015

Vijana wakamatwa kwa uhalifu Dar

Jeshi la polisi nchini Tanzania linawashikilia baadhi ya vijana wanaotuhumiwa kufanya vurugu kwa kuwapora watu mali.Kundi la  kihuni la vijana linalojulikana kama ''Panya Road'' lilifanya vurugu kwa kuwapora watu mali zao na kwenye maduka ya mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.Msemaji wa jeshi la Polisi nchini

Air Asia:Miili 37 imepatikana mpaka sasa


Shirika la uokoaji nchini Indonesia limesema hivi sasa miili 37 imepatikana kutoka kwenye bahari ya Java ambapo ndege ya Air Asia iliangukia mwishoni mwa juma lililopita.Helikopta na Meli za kijeshi zimekuwa zikifanya doria katika eneo la bahari hiyo ambapo vitu vinavyoelezwa kuwa mabaki ya ndege