News

Msako unaendelea  kuwatafuta  wauaji  wa  watu  12  

Katika shambulio  lililotokea  katika  ofisi  za  jarida  la Charlie Hebdo  mjini  Paris  siku  ya  Jumatano. Polisi  wanatafuta katika  maeneo  ya  vijijini watuhumiwa  wawili, Cherif  na Said Kouachi, ambao  wanaripotiwa  wamefanya  uporaji katika  kituo  kimoja  cha  petroli. Ufaransa  umekuwa na siku ya kwanza  ya  maombolezo  jana  Alhamisi ikiwakumbuka  wale waliopoteza  maisha  katika  mauaji hayo, ikiwa  ni  pamoja  na  polisi  mwanamke ambaye alipigwa  risasi  mtaani.
Maafisa  nchini  Ufaransa wamesema  hakuna  ushahidi wa uhusiano  kati  ya mauaji  ya  Charlie Hebdo  na shambulio la  pili  siku  ya  Alhamisi. Polisi mwanamke  alipigwa  risasi katika  eneo  la  Montrouge  kusini  mwa  mji mkuu Paris

Yatsenyuk akutana na Merkel mjini Berlin

Kansela  wa Ujerumani Angela  Merkel  amesema  vikwazo dhidi  ya Urusi vitaondolewa tu pale ambapo makubaliano  ya  amani yatatekelezwa  na  pande  zote  mbili  katika  mzozo  huo  nchini Ukraine. Merkel  ametoa matamshi  hayo  wakati  wa  mkutano  wa pamoja  na waandishi habari mjini  Berlin pamoja na waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk.  Chini  ya  makubaliano ya  Septemba mwaka uliopita, Ukraine  na   waasi  wanaoiunga  mkono  Urusi walikubaliana  kusitisha  mapigano, lakini  yameshindwa kuzuwia mapigano  zaidi.
Merkel  ameweka  msimamo  sawa  kwa  kusema vipengee  vyote vya  makubaliano  ya  Minsk ni  lazima  vitimizwe na mkutano  mjini Astana utakuwa  na  maana  kwamba  vipengee  vyote  hivyo vitatimizwa  mara  moja. Mazungumzo  zaidi yamefanyika  mwezi Desemba  kuweza  kupatikana  kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, hata  hivyo, yalivunjika  na  kusababisha makubaliano  ya kubadilishana  wafungwa.

http://www.bbc.co.uk/swahili














No comments:

Post a Comment